googleAds

JICA wajitosa kudhamini riadha wanawake

NA ZAINAB IDDY

TAASISI ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan(JICA), imejitosa kudhamini michuano ya riadha kwa wanawake iliyopangwa kufanyika wikiendi hii, kwenye  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Michuano hiyo iliyoanzishwa mwaka juzi inaanadaliwa na Shirikisho la Riadha Tanzania(RT) kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Akizungumza Dar es Salaam jana,  Kaimu katibu mkuu wa BMT, Neema Msitha, alisema michuano hiyo itashiriki mikoa 31 ikiwamo mitano kutoka Zanzibar.

Neema alisema lengo la michuano hiyo ni kuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike katika michezo ikiwamo riadha, lakini kutoa fursa kwa wanariadha wa kike kuonesha vipaji vyao.

“Mwaka huu tunatarajia kutakuwa na washiriki zaidi ya 200  na viongozi wao wanapewa nafasi ya kukimbia, lakini tumewapa mwaliko wanariadha kutoka Sudan Kusini ili kuja kuongeza ushindani.

” BMT tunampongeza sana mwanariadha mstaafu Juma Ikangaa, ambaye ni kiunganishi kati ya BMT na JICA kwa kufanikisha mradi huu wa mbio za wanawake hapa nchini,” alisema Neema.

@@@


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*