Jay Z aunda mfuko kusaidia familia ya Nipsey

LOS ANGELES

RAPA Shawn Carter, maarufu kama Jay Z, ameunda mfuko ambao atachangia kiasi cha dola za Marekani milioni 15, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 34.7 kwaajili ya kusaidia watoto wa marehemu Nipsey Hussle, aliyefariki dunia wiki hii kwa kupigwa risasi huko Los Angeles, Marekani.

Jay Z, ambaye alimsaini Nipsey katika lebo yake ya Roc Nation, ameweka wazi kuwa mfuko huo utasimamiwa na mke wa marehemu, Lauren London na utawasaidia watoto wao, Eman na Kross.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*