Jay Dee awapa dili wabunifu wa mavazi

NA BRIGHITER MASAKI

STAA wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’, amewapa nafasi wabunifu wa mavazi na mapambo ya kushiriki katika maandalizi ya video yake mpya anayotarajia kuifanya leo nchini Afrika Kusini.

Jay Dee ambaye alitoa dili hilo juzi, amesema tayari amepokea maombi ya wabunifu wa mavazi na wanamitindo wengi kutoka Tanzania ambao atafanya nao katika video yake hiyo inayotarajia kutikisa chati za muziki Bongo.

 “Nitarekodi video yangu ya kwanza kwa mwaka 2019 nchini Afrika Kusini, kuanzia Alhamisi (juzi) mpaka leo hii jioni, naendelea kukaribisha wabunifu wapya wa mavazi na mapambo,” alisema Jide.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*