googleAds

James kupewa muda kupumzika

MANCHESTER, EnglandĀ 

KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, atampumzisha winga wake kinda, Daniel James, ili kujifua zaidi kwa mujibu wa ripoti.

James mwenye umri wa miaka 21, mara kadhaa alichezewa rafu na mabeki wa timu pinzani, jambo ambalo limempa hofu kocha wake.

Winga huyo huenda akakosa mechi ya Ligi Kuu England mwishoni mwa wiki, Man United itakapowakaribisha Brighton kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*