googleAds

James amzawadia baba yake bao

MANCHESTER, England

WINGA mpya wa Manchester United, Daniel James, amemzawadia bao baba yake mzazi ambaye alifariki Dunia miezi michache iliyopita, baada ya kufunga akitokea benchi.

James alifunga bao hilo kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea, wikiendi iliyopita ambapo Man United ilitoka na ushindi wa mabao 4-0.

Nyota huyo raia wa Wales, baada ya kupachika bao hilo, alishangilia kwa huzuni, huku akiangalia angani na kunyoosha mikono yake juu.

Baba yake alifariki siku chake baada ya kukubali kujiunga na Mashetani Wekundu hao, kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 18 (sh bil.49) akitokea Swansea City.

Naye kiungo wa klabu hiyo, Scott McTominay, alimsimfu winga huyo, akisema anajivunia kucheza naye pamoja katika kikosi hicho.

“Huyu ndio kijana wangu, najivunia kwa kile alichofanya,” alsiema McTominay.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*