INIESTA RASMI KUCHEZA JAPAN

BEIJING, China


 

 

KIUNGO Andres Iniesta, amekamilisha usajili wake kwa kujiunga na Vissel Kobe ya Ligi Kuu ya Japan, timu inayomilikiwa na wadhamini wa Barcelona, Rakuten.

Iniesta amesaini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo ikiwa ni wiki moja imepita tangu alipoaga Barca.

Mbali ya kucheza, pia mkongwe huyo atashirikiana na wataalamu wengine wa timu za vijana klabuni hapo.

Ieleweke kuwa Iniesta anakuwa mchezaji wa kwanza mwenye jina kubwa kutua Japan tangu Gary Lineker aliposajiliwa na Nagoya Grampus Eight mwaka 1992.

Picha iliyosambaa zaidi ni ile ya ‘mido’ huyo akiwa na bilionea, Hiroshi Mikitani, ambaye ndiye mmiliki wa Vissel na Kampuni ya Rakuten inayoidhamini Barca.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*