googleAds

Iheanacho akumbukwa Super Eagles

LAGOS, Nigeria

MSHAMBULIAJI wa Leicester City, Kelechi Iheanacho, ameitwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’ kitakachoivaa Ukraine Septemba 10, mwaka huu.

Iheanacho aliachwa katika kikosi kilichoshiriki fainali za Afcon 2019 zilizofanyika nchini Misri, lakini sasa cheche alizoonesha ‘pre-season’ akiwa na kikosi cha Leicester City, zimempa shavu.

Nyota wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Wilfred Ndidi, Ahmed Musa, Henry Onyekuru na Samuel Chukwueze.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*