Ibrahimovic ajengewa sanamu Sweden

STOCKHOLM, Sweden 

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic, amejengewa sanamu ya heshima ambalo limezinduliwa katika mji wa Malmo alipozaliwa.

Mashabiki wengi walifurika kulishuhidia sanamu hilo chini ya Shirikisho la Soka la Sweden (FA).

Ibrahimovic ameshikilia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Sweden.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Ibrahimovic alisema amejivunia heshima hiyo na hataisahau katika maisha yake.

Kwa sasa nguli huyo anakipiga katika klabu ya LA Galaxy ya Marekani ambayo alijiunga nayo mwaka jana akitokea Manchester United. 

Ibrahimovic amefunga jumla ya mabao 400 akiwa amechezea klabu mbalimbali zikiwamo Barcelona, Paris-Saint Germain na Manchester United.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*