googleAds

HISTORIA YA UWANJA UTAKAOCHEZEWA FAINALI YA LIGI YA MABINGWA ULAYA

Cardiff, Wales

PAMOJA na kuwepo kwa viwanja vingi vya kwenye mataifa mbalimbali, lakini Uwanja wa Millennium uliopo mjini Cardiff nchini Wales, ambao utachezewa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Juni 3 mwakani una historia ya kipekee sana.

Upo kwenye ziwa Taff katikati ya mji wa Cardiff. Uwanja huo umekuwa kivutio kikubwa kutokana na eneo uliopo na michuano ya ragbi iitwayo ‘Six Nations Championship’ hufanyika kila mwaka, hivyo watu wengi huudhuria na kufurahia.

Lakini wasichojua wengi ni kwamba uwanja uko kwenye eneo ambalo lina historia kubwa, ambapo uwanja huo ulipewa jina hilo ambalo zamani lilikuwa ni la hoteli, ambayo kwa sasa inaitwa

Angel. Ambapo hoteli ya zamani iliyopo kwenye sehemu hiyo ya uwanja ilivunjwa mwaka 1870, ila jina lake mpaka sasa linaishi kupitia uwanja huo.

Kulikuwa na mpango wa kuuvunja uwanja huo ambao miaka ya 1853 uliitwa Cardiff Arms Park ili kujenga kituo cha reli pembezoni mwa uwanja huo, lakini wazo hilo halikufanikiwa kutokana na kutumiwa na timu nyingi za rugby na soka kama Cardiff ambao baadaye mwaka 1910 walijenga uwanja wao uitwao Ninian Park.

Majukwaa mapya ya uwanja huo yalijengwa mwaka 1885, lakini yolisombwa na mafuriko mwishoni mwa karne ya 19, kabla ya uwanja huo kupata umaarufu mkubwa kufuatia timu ya Wales ya ragbi kufanya vizuri mwanzoni mwa karne ya 20, ambapo timu hiyo haikufungwa kwenye uwanja huo wa Arms Park kwa miaka 12.

Miaka ya 1930 chama cha ragbi cha Wales kilitaka kuutosa uwanja huo wa Cardiff Arms Park, lakini baada ya mazungumzo waliamua kujenga majukwaa mapya, likiwemo lile la Kaskazini na vyumba vipya vya kubadilishia nguo.

Mwaka 1939 uliharibiwa vibaya na Vita ya Pili ya Dunia, kabla ya ardhi yake kuharibiwa tena na mabomu ya Ujerumani mwaka 1941, huku jukwaa la Kaskazini liliharibika kabisa pamoja na lile la Kusini na lile la West Terrace, hadi mwaka 1950 majukwaa hayo yalipojengwa upya. Kuharibika kwa ardhi ya uwanja huo kulisababisha kujaa kwa maji na kuwepo na mafuriko.

Ilipita miaka kadhaa hadi kupatikana kwa Uwanja wa Millennium na miaka mingine 12 uwanja huo kuweza kupendwa ukiwa umegharimu karibia pauni milioni 150 na kuufanya uwanja huo wa kipekee.

Uwanja huo una uwezo wa kufunuliwa na kufunikwa kwa dakika 20, ikiwa ni uwanja wa pili wenye uwezo wa kufunikwa eneo kubwa baada ya Uwanja wa Cowboys mjini Texas, Marekani, pia una sehemu maalumu za kupandia majani ili kuyatumia wakati majani ya uwanja yatakapokuwa yameng’oka au kuharibika.

Baada ya uwanja huo kumalizika, mechi ya kwanza ilikuwa ni ya timu ya taifa ya ragbi ya Wales na Afrika Kusini, ambapo Wales walishinda pointi 29 kwa 19. Mechi mbalimbali zilichezwa kwenye uwanja huo, zikiwemo fainali mbili za Kombe la Dunia la Ragbi kwa kipindi kifupi.

Kwa upande wa timu ya taifa ya soka ya Wales, walicheza mechi yao ya kwanza kwenye uwanja huo mwaka 2000, Jari Litmanen akifunga bao la ushindi walipoichapa Finland 2-1.

Tangu uwanja huo wa Millennium ulipofunguliwa umekuwa ukifanyika maonyesho mbalimbali ya muziki, mechi za soka, mapambano ya ngumi na kuufanya kuwa moja ya uwanja mkubwa na wa kuvutia kwa matukio mbalimbali duniani.

Uwanja huo ulifanyika fainali sita za Kombe la FA, kuanzia mwaka 2001 hadi 2006 wakati Uwanja wa Wembley unafanyiwa ukarabati, ambapo Arsenal walibeba mataji mara tatu kwenye uwanja huo, huku Liverpool mara mbili.

Pia zilifanyika fainali za Kombe la Ligi na kuwa na gundu kwa timu zilizokaa vyumba vya wageni, ambapo mataji 11 ya michuano hiyo yalibebwa na timu iliyokaa vyumba vya upande wa wenyeji.

 

TAKWIMU ZA MSIMU HUU

IDADI YA MABAO KWENYE KILA DAKIKA

Dakika 1 hadi 15 mabao       42

Dakika 16 hadi 30 mabao 47

Dakika 31 hadi 45 mabao 41

Dakika za nyongeza (kipindi cha kwanza) mabao 9

Dakika 46 hadi 60 mabao 49

Dakika 61 hadi 75 mabao 31

Dakika 76 hadi 90 mabao 48

Dakika za nyongeza (kipindi cha pili) mabao 11

Jumla mabao 278

 

 

WAFUNGAJI

10   Lionel Messi      Barcelona

6     Edinson Cavani PSG

5     Robert Lewandowski Bayern

4     Arda Turan Barcelona

4     Aubameyang     Dortmund

4     Dries Mertens    Napoli

4     Riyad Mahrez    Leicester

4     Karim Benzema       Real Madrid

4     Mesut Ozil  Arsenal

 

 

PASI ZA MABAO

7     Neymar       Barcelona

4     Ousmane Dembele  Dortmund

4     Eduardo Salvio Benfica

4     Cristiano Ronaldo    Real Madrid

3     Dries Mertens    Napoli

3     David Alaba      Bayern

3     Luis Suarez Barcelona

3     Andriy Yarmolenko       Dynamo Kyiv

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*