HII MIJEZI YA TWIGA INABIDI NIIFUE TU

TEH teh teh! Hivi yule Neima wa akina Chirwa ni mwanamke au mwanaume maana si kwa vitu adimu vile. Mwanamke gani anatoka mbio kiasi kile na ile miskilizi kama kwenye yutubu sijui kaitoa wapi.

Ikija kulia yumo, ikija kushoto yumo. Yaani anavuruga tu, haeleweki kabisa pale baada ya mchezo sasa ilibidi nishuke fasta nikamwangalie vizuri, bado macho yangu yalikataa kama yule mwanamke zaidi ya sauti yake kuwa nyororo lakini sura sasa, loh!

Dah! Ndo hivyo bhana kama mlivyosikia, mgonjwa katema dawa. Wakati mwingine hata mimi nakuwa na huruma asee, maana si kwa yale niliyoyaona pale kwa Mchina.

Hivi yule dada’ke Chirwa aliyevaa mjezi namba 11 kama Neima mbona ana balaa vile, alikuwa anateleza kadiri alivyokuwa anataka tena uwanja wenyewe una nyasi za kuslaidi ndo kabisa alifanya mambo makubwa.

Lakini hata mimi nilijiuliza hivi yule ni mwanamke kweli maana pale kwenye chesti pako emte kabisa. Hakuna hata dalili za kusema zitatokea mwaka ujao yaani ilinichanganya akili tu.

Kutokana na kiwango cha siku ile kilichoonyeshwa na wale Twiga kimoyomoyo nilisema ntasubiri mchezo wa marudiano nione kama nitapata muda wa kuifua mijezi yao au niwapotezee.

Haya sasa na kule wamepata sare ya 1-1, lakini wameshindwa kusonga mbele sababu waliruhusu kufungwa mabao matatu hapa homu. Lakini fresh tu, kwa yale niliyoyasikia kuhusu timu hiyo inasikitisha bhana.

Mbona jezi zao ni chafu sana, kuna mambo ya maajabu sana yanatokea asee, lakini yapo chini ya kapeti tu pamoja na uchafu wote mi nitajitahidi kuzifua jezi hizo hadi ziwe safi tu.

Teh teh teh hatari tupu asee, kumbe hata mechi zenyewe zimechezwa basi tu. Pale tifua tifua walishindwa kabisa kuwapa michezo ya kirafiki kama walivyofanya kwa kaka zao wadogo wale.

Malalamiko kibao yaani, kambi yenyewe waliyokaa ilikuwa haieleweki kwa kuwa lilikuwa suala la taifa waliamua kujitolea tu. Ndio ilikuwa hivyo, punda afe mzigo ufike. Hakukuwa na namna asee.

Hakunaga mwizi mvivu bhana! Tatizo tumekuwa tukikosea kila siku makosa yale yale kwa hawa wadada. Lakini muda mwingine nasikia hata wao wenyewe wanaelemewa na joto asee kiasi cha kukutana wenyewe kwa wenyewe.

Ooh! Hata wao wana mioyo bhana, kuhusu kupenda tu, hata mimi mjezinho napenda japo kazi yangu kufikicha miuchafu hii hadi itoke. Ila nasikia wamezidisha asee sasa hapa inabidi wapunguze.

Isije ikawa shida kubwa sana hata kwenye kupiga mpira. Hehehe mambo ni hiviii, lakini mambo machafu yote yanaanzia tifua tifua kushindwa kutoa kipaumbele kwa hawa wadada kama wanavyofanya kwa timu kubwa ya wanaume na vijana.

Ahadi yangu iko palepale hii mijezi yao nitaifua, nitahakikisha inatakata kweli na kila kitu kitaenda sawa. Presha ishashuka sasa.

Unajua ile juzi kiroho kilikuwa kinadunda sana asee, ile kumwona Ninja tu kwenye kikosi nikajua hapa lazima kutakuwa na kareti tu, maana amekuwa mtu wa matokeo yule jamaa.

Lakini wazee wa Jangwani bhana waliamua kutupa raha tupu baada ya kuharibu ile siku ya Pasaka. Hivi ni kweli wale wauza mafuta ya alizeti ni ndugu zenu kweli?

Kila mkikutana nao wanabana, kila mkijaribu wanabana mwisho wa siku wakawatoa. Inabidi nifanye uchunguzi wa kina asee kuhusu hilo, haiwezekani undugu uharibiwe kiasi hiki cha kukoseshana raha mtaani.

Ile migoli ya kikatili sana mapema tu nasikia soma ubao, ooh mara kipindi cha pili mapema tu tena nasikia lingineeee teh teh teh Yanga bhana mi nawasubiri warudi kutoka huko Dicha kwanza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*