Hellen Sogia kuweka wakfu kazi zake

NA BRIGHTER MASAKI

MWIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini na mtumishi wa Mungu, Hellen Sogia, anatarajia kuweka wakfu kazi zake mbalimbali Julai 7, mwaka huu katika Ukumbi wa B. Mellin (Tumbi), Kibaha mkoani Pwani.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Helles Sogia alisema tukio hilo maalumu la kihistoria katika maisha yake ya utumishi kama ambavyo alivyoitwa na kuagizwa na Mungu, litasindikizwa na kwaya mbalimbali, watumishi na waimbaji binafsi, hivyo watu wote wanakaribishwa.

“Kazi ambazo zitawekwa wakfu siku hiyo ni nyimbo (Zaburi, Sifa na Kuabudu), mafundisho kwa njia ya vitabu, mitandao na CD, utumishi ambalo ni kusudio nililopewa na shughuli yote hii itasimamiwa na watumishi wa Mungu kutoka kwenye huduma mbalimbali,” alisema Hellen.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*