googleAds

HAZARD: NILICHOWAFANYA LIVERPOOL SITOKISAHAU

LONDON, England


 

WINGA wa timu ya Chelsea, Eden Hazard, amelisifia bao alilowafunga Liverpool katika mechi ya mtoano ya Kombe la Carabao, iliyochezwa usiku wa kuamkia jana, kuwa ni moja ya mabao yake bora aliyowahi kuyafunga.

Hazard alitokea benchi na kuisaidia Chelsea kuondoka na ushindi kwenye mchezo huo uliochezwa dimba la Anfield, wakitoka nyuma na kuinyuka Liverpool mabao 2-1, huku Mbelgiji huyo akipachika bao la ushindi.

Bao la kwanza la Chelsea lilifungwa na beki Emerson Palmieri dakika ya 79, akiunganisha krosi ya Hazard, kabla ya winga huyo kumpiga tobo Roberto Firmino, wakati akitengeneza shambulizi na kuachia fataki kali lililotinga wavuni.

“Kuna baadhi ya mabao niliyafunga kama hilo, si mara nyingi sana. Lina haki ya kuwa katika orodha ya mabao yangu matatu bora zaidi niliyowahi kuyafunga.

“Nakumbuka niliwafunga Arsenal bao kali miaka michache iliyopita. Hili la leo (juzi) nalo zuri mno. Hasa ukiifunga timu kubwa, kitu ambacho ndio muhimu zaidi,” alisema Hazard.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*