GUARDIOLA: NATAMANI NIWEPO KOMBE LA DUNIA

MANCHESTER, England


 

KOCHA wa timu ya Man City, Pep Guardiola, amefunguka nia yake ya kuanza kufundisha ngazi ya kimataifa na siku moja kuinoa timu inayoshiriki Kombe la Dunia.

Guardiola mwenye umri wa miaka 47, amenasa mafanikio makubwa katika timu za Barcelona, Bayern Munich na Man City, ambayo ametwaa nayo ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2017-18.

“Nataka nifundishe timu yoyote kwenye Kombe la Dunia au Kombe la Mataifa Ulaya.

“Ingawa nafahamu kwa miaka ijayo nitakuwepo hapa (City), lakini sijafunga milango kwa timu yoyote inayonihitaji, bado umri wangu unaruhusu,” alisema.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*