Guardiola atishia nyau Man City

MANCHESTER, England 

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amesisitiza ataondoka msimu ujao endapo klabu hiyo haitatimiza mipango yake ambayo ameiweka.

Kwa mujibu wa gazeti la Sun, Guardiola ana imani kikosi hicho kitatetea ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

“Wanafahamu fika nitaondoka mambo yakienda hovyo Man City, hata hivyo nitapambana mambo yaende kama nilivyopanga, sitokubali mambo yasiyo sawa yaendelee kwenye timu,” alisema Guardiola.

Wikiendi iliyopita Man City ikicheza nyumbano, ilipokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Wolves, kitendo ambacho kilimkera kocha huyo raia wa Hispania. 

Aidha kipigo hicho ambacho ni cha pili msimu huu kinaifanya Man City kuachwa nyuma kwa pointi nane na vinara wa ligi Liverpool.

Itakumbukwa msimu uliopita, Guardiola alichukizwa na baadhi ya wachezaji wake, ambao walihudhuria pati moja jijini Manchester na kulewa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*