GUARDIOLA AJIPA MATUMAINI KWA MAJERUHI  DE BRUYNE

 

LONDON, England

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema kwamba ana matumaini majeraha aliyoyapata juzi staa wake, Kevin De Bruyne, wakati wa mchezo wa Kombe la EFL ambao waliondoka na ushindi dhidi ya Fulham,  hayatakuwa makubwa sana.

Nyota huyo raia wa Ubelgiji alikumbana na majeraha ya goti Agosti mwaka huu na yakamfanya akae nje ya uwanja kwa muda wa miezi miwili na mchezo huo dhidi ya Fulham ulikuwa ni wa pili.

Staa huyo aliweza kucheza kwa muda mwingi wa mtanange huo ambao Man City waliondoka na ushindi wa mabao 2-0, lakini ikalazimika kumpumzisha dakika za mwisho baada ya kuangukiwa na nyota wa Fullham, Timothy Fosu-Mensah.

“Kevin alifanyiwa uchunguzi na madaktari,” Guardiola aliwaambia waandishi wa habari.

“Siwezi kufahamu jinsi ukubwa wa jeraha ulivyo. Hakitafaa kitu chochote kama tatizo ni kubwa,” aliongeza kocha huyo.

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*