Gharama zamfanya Dj Cyp afungue studio Marekani

DALLAS, MAREKANI

MSANII, Dj na mtayarishaji wa Bongo Fleva anayeishi Dallas Texas, Marekani, Patrick Cypian ‘Dj Cyp’, amesema alipohamia nchini humo alishindwa kurekodi kutokana na gharama kubwa ya studio.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Dj Cyp anayemiliki studio  za Handzdown Records zilizopo Dallas, alisema alipokwenda Marekani kusoma mwaka 2001, alikaa muda mrefu bila kurekodi ndiyo maana akafungua studio ili wasanii wengine wasikutane na changamoto alizozipitia.

“Napenda kurap, ku DJ vilevile na ku prodyuzi muziki, lakini muda ni jambo la muhimu sana, nilipokuja Marekani nilishindwa kurekodi ngoma hata moja, gharama zipo juu sana, ndiyo maana nikaamua kujenga studio ili niwasaidie wasanii wengine,” alisema Dj ambaye ni memba wa zamani wa kundi la hip hop nchini, Jungle Crewz Posse.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*