Gervinho tupa kule Afcon 2019

JAMUSUKRO, Ivory Coast

STAA wa zamani wa Arsenal, Gervinho, ametemwa katika kikosi cha mwisho cha timu ya taifa ya Ivory Coast kinachojiandaa kwa fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019) zinazotarajiwa kuanza Juni 21, mwaka huu, nchini Misri.

Nyota huyo amewekwa kando licha ya mabao yake 11 na ‘asisti’ nne katika mechi 30 za Serie A akiwa na Parma msimu uliopita.

Ivory Coast wataivaa Uganda Juni 14, kabla ya kuwashukia Ethiopia siku nne baadaye, ikiwa ni sehemua ya kujiandaa na michuano hiyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*