googleAds

Gattuso amtakia heri Ancelotti

MILAN, Italia 

KOCHA mpya wa Napoli, Gennaro Gattuso, amemtakia maisha mema, Carlo Ancelotti, aliyekuwa kocha wa miamba hiyo ya Italia.

Ancelotti alifungashiwa virago ikiwa ni siku moja tu baada ya Napoli kufuzu hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiifunga Genk mabao 4-0.

“Ancelotti namchukulia kama baba yangu mzazi, siku zote nimekuwa karibu naye kwa mambo mengi, amekuwa akiniunga mkono kwa kila jambo ninalofanya, na nina mheshimu sana,” alisema Gattuso.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*