FRED AAMSHA HASIRA ZA MASHABIKI LIVER

LONDON, England


 

NYOTA  mpya wa Manchester United, Fred, ameamsha hasira za mashabiki wa Liverpool baada ya kuchaguliwa kwenye kikosi cha kwanza cha Brazil ambacho mwishoni mwa wiki kiliibuka na ushindi dhidi ya Marekani.

Katika mchezo huo wa kimataifa wa kirafiki ambao Brazil waliibuka na ushindi wa mabao  2-0  dhidi ya Marekani, Fred alichezeshwa nafasi ya kiungo sambamba na mastaa wenzake, Casemiro  na  Phillipe Coutinho.

Hata hivyo, hapakuwapo na nafasi kwa kiungo mpya wa  Liverpool, Fabinho na badala yake akapangwa kucheza kama beki wa kulia.

Kutokana na  Fabinho kupangwa katika nafasi hiyo ya beki, ilionekana kuwakera mashabiki wengi wa Liver ambao wengi wao walisikitika kwa kuona nyota huyo ambaye ameigharimu timu hiyo pauni milioni 39 akichezeshwa nafasi tofauti na ile ya kiungo mkabaji aliyoizoea.

Kupitia ujumbe ambao waliutuma kupitia mitandao yao ya kijamii, mashabiki wengi wa  Liverpool wanaamini nyota wao huyo mpya alitakiwa kuchezeshwa katika safu ya kiungo badala ya nyota huyo wa Man Utd.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*