FLAVIANA MATATA, NICK MINAJ WAKUTANA ANA KWA ANA

NA CHRISTOPHER MSEKENA


 

MWANAMITINDO wa Tanzania anayeendelea kufanya vizuri kwenye anga za kimataifa, Flaviana Matata, hivi karibuni amekutana na rapa wa nchini Marekani, Nick Minaj, katika hafla ya utolewaji wa tuzo za mitindo (Fashion Media Awards 2018) jijini New York.

Agosti 21 mwaka huu, Flaviana alitangaza kupata dili la kuzipamba kucha za mrembo huyo katika picha alizopiga ili kupamba jarida la mitindo Vogue Arabia.

Nick Minaj, alitumia bidhaa za rangi za kucha za Flaviana Lavy namba 29 hivyo kuwa ni hatua kubwa ya mafanikio kwa mwanamitindo huyo kibiashara.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*