googleAds

FIESTA 2018… ITAKUWA HATARI NDANI YA SONGEA

NA MWANDISHI WETU


 

VUMBI la tamasha la Tigo Fiesta 2018, litaendelea kutimka leo kwenye mjini Songea.

Hili litakuwa ni onyesho la nne la tamasha hilo linaloandaliwa na Kampuni ya Clouds Media Group na kufanyika kila mwaka katika mikoa mbalimbali nchini, baada ya kuanzia Morogoro, Sumbawanga na Iringa.

Tamasha hilo ambalo linadhaminiwa na Kampuni ya Mtandao wa Mawasiliano wa Tigo na mwaka huu limepewa kaulimbiu ya ‘Vibe Kama Loteeeee!.

Wasanii mbalimbali watakaokamua kwenye onyesho hilo ni Lulu Diva, Mr Blue, Fid
Q, Roma Mkatoliki na Stamina ‘Rostam’, Weusi, Chegge, Barnaba, Mesen Selekta, Foby, Zaid, Ruby na wengineo wa mjini Songea.

Katika tamasha lililofanyika mjini Iringa, wasanii waliopanda jukwaani walifanya shoo kabambe iliyokonga nyoyo za wakazi wa mji huo na maeneo ya jirani.

Akizungumza mbele ya umati wa mashabiki waliohudhuria tamasha hilo kwenye uwanja huo wa Samora, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela, aliipongeza kampuni ya Tigo kwa kuwapelekea burudani na fursa mbalimbali kwa wakazi wa Iringa.

“Hii ni fursa ya pekee kwa wakazi wa mji huu ambayo kampuni ya Tigo imetuletea kwa mara nyingine ndani ya mkoa huu. Ukiondoa burudani, pia wafanyabiashara wamenufaika sana ndani ya wiki nzima,” alisema Kasesela.

Pia, mkuu huyo wa wilaya alipata nafasi ya kumkabidhi zawadi ya keki msanii Chege Chigunda kwa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake.

Kwa upande wa burudani, wasanii wa kundi la Weusi ndio waliofunika kwenye tamasha hilo ilipopelekea mashabiki kuomba wasitoke kwenye jukwaa na kundi la Weusi walifanya hivyo hadi mwisho wa shoo kwa kuimba nyimbo zao nyingi za kuvutia zikiwemo, Madaraka, Swagire, NiCome na nyingine nyingi.

Akizungumzia tamasha la Iringa, Katibu Mkuu wa Kamati ya Maandalizi ya Tigo Fiesta 2018, Gardner G. Habash, aliwahakikishia burudani ya hali ya juu wote watakaohudhuria tamasha hilo mjini humo.

“Katika miaka ya hivi karibuni, tumetambua mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii unaotokana
na tamasha la Tigo Fiesta. Mbali ya kutoa fursa ya kuutangaza mkoa husika, pia inaongeza idadi ya wageni na kusababisha ongezeko kubwa la fursa za biashara kwa wamiliki wa hoteli, migahawa, mama ntilie, vyombo vya usafiri kama vilebodaboda,kumbizastarehe na biashara nyinginezo,” alisema Habash.

Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga, alisema: “Tigo inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia
Tigo Pesa Masterpass QR. Tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo
wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu Sh 5,000 pekee badala ya Sh 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslimu.

“Wateja wanapaswa kupiga *150*01# nakuchagua5(lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.”

Mpinga aliongeza: “Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za Sh 100,000, zawadi za kila wiki za Sh milioni moja, simu janja za mkononi zenye thamani ya Sh 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la Sh milioni 10 kwa mshindi wa jumla.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*