Ferooz asimulia kupoteza mil 100/- kwenye madini

NA JEREMIA ERNEST

MKONGWE wa Bongo Fleva aliyewahi kutamba na nyimbo kadhaa ukiwamo wa  Starehe, Feruzi Mrisho ‘Ferooz’, amesema alipotea kwenye muziki baada ya kujiingiza kwenye biashara ya madini iliyompotezea fedha nyingi.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Ferooz alisema kwa sasa amerudi tena na wimbo wake mpya wa Mapigo ambao ameufanyia maboresho makubwa ya utunzi na uimbaji, hivyo anaamini mashabiki watampokea.

“Nikweli nilipotea kwa sababu nilijikita katika biashara ya madini, muda wa kufanya muziki nilikosa kwa sababu ya kusimamia biashara, lakini sikupata mafanikio zaidi ya kupoteza fedha zangu zinakaribia Shilingi 100,000,000,” alisema Ferooz.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*