FERDINAND: SALAH KWA RONALDO? UTANI HUO

LONDON, England

BEKI wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand, amesema ni mapema kumfananisha Mohamed Salah wa Liverpool na Cristiano Ronaldo.

Jumanne ya wiki hii, Salah alifunga mara moja katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City, na lilikuwa la 39 tangu kuanza kwa msimu huu.

Kwa upande wa Ronaldo, ameshaziona nyavu mara 40 katika mechi 37 alizocheza.

“(Salah) anafanya vizuri. Salah anazungumziwa kwa kuwa na msimu mzuri lakini atahitaji misimu mingine 15 kumfikia (Ronaldo),” alisema.

Mkataba wa Salah unatarajiwa kufikia tamati Juni, 2022, huku ule wa Ronaldo na Real Madrid ukimalizika Juni, 2021.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*