googleAds

FARAH ATISHA MBIO ZA MITA 5000, ATINGA FAINALI IAAF

download (4)

LONDON, England

MKALI wa riadha wa England, Mo Farah amefanikiwa kutinga fainali mbio za dunia jijini London baada ya wiki hii kushinda mbio ngumu za mita 5000.

Farah alikumbwa na changamoto ya mvua katika mbio hizo sambamba na maumivu ya goti la mguu wake wa kushoto, lakini anatarajiwa kuonesha makali yake tena kwenye fainali ya kesho Jumamosi.

Farah mwenye umri wa miaka 34, alimaliza nafasi ya tatu kwa kutumia muda wa dakika 13 na sekunde 30.18 na alijikatia tiketi ya kushiriki fainali kesho huku akiwa na matumaini ya kushinda medali mbili dabo za mita 5000/10,000 kwa mara ya tano mfululizo.

“Mbio zilikuwa ngumu mno. Baridi lilinitesa lakini misheni ilitimia. Kwa kiasi fulani najisikia vizuri kwenye goti ingawa nina uchofu,” alisema Farah.

“Ni kitu kigumu sana kushinda medali dabo, nadhani mlimuona hata Usain Bolt. Ingekuwa vizuri kumuona akiibuka mshindi lakini ndio hivyo tena. Kama nikishinda basi itakuwa historia ya kupendeza na nimejipanga maana sidhani kama wapinzani wangu watanichukulia poa,” aliongeza Farah.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*