googleAds

Eymael ajitetea kwa Yikpe, Mkwasa naye amshangaa

TIMA SIKILO NA ZAINAB IDDY

WAKATI Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael akijitetea kuhusiana na kiwango cha mshambuliaji wao, Yikpe Gislain, msaidizi wake, Charles Mkwasa, amemshangaa nyota huyo, raia wa Ivory Coast.

Yikpe, alisajiliwa na Yanga kipindi cha dirisha dogo msimu huu, akitokea Gor Mahia ya Kenya, hadi sasa ameshindwa kuonyesha kiwango cha juu, kiasi cha kuwakera mashabiki wa timu yake hiyo mpya.

Akizungumza na BINGWA jana, Eymael alisema japo amekubali kupokea lawama kutokana na kiwango cha mchezaji huyo, lakini ifahamike kuwa yeye si aliyemsajili.

Eymael alisema ikiwa mchezaji anayetakiwa kucheza nafasi ya Yikpe ni David Molinga na Tariq Seif ambao ni majeruhi, hawezi kumwepuka Muivory Coast huyo.

“Yikpe hajafanya vizuri, sawa, lakini mfano mzuri ni mchezo wa Polisi, mabao hayakutokea kwake, lakini anatimiza majukumu yake, haina haja ya kumlaumu kwani ndiye mshambuliaji tuliyenaye.

“Wakinilaumu kwa kumtumia, sawa, lakini wanapaswa kufahamu mimi sijamsajili Yikpe, nimemkuta na kama sina wa kumtumia, lazima nimtumie yeye,” alisema.

Kwa upande wake, Mkwa sa alisema: “Mara nyingi najiuliza tatizo ni nini, kwani mazoezini anafanya mazoezi na kuonekana bora, lakini akipangwa katika mechi, anashindwa kuonyesha kile alichokifanya katika mazoezi.

“Nafikiri anahitaji muda, lakini pia huenda presha ya mashabiki na maneno yanayozungumzwa dhidi yake yanamkatasha tama… naamini akishazoea na kukubali changamoto, atakuwa mzuri sana.”

Hadi sasa, Yikpe amefunga mabao mawili, moja la Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United na lingine akiifunga Iringa United, ukiwa ni mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*