Emery: Aubameyang pambana baba

LONDON, England

KOCHA wa Arsenal, Unai Emery amemtaka straika wake, Pierre-Emerick Aubameyang kuendelea kucheka na nyavu ili msimu huu aweze kuibuka mfungaji bora wa michuano ya Ligi Kuu England.

Kwa sasa Aubameyang ndiye anayeshika usukani kwenye msimamo wa wafungaji bora na mabao mawili aliyoifungia  Arsenal katika ushindi wao dhidi ya Tottenham mwishini mwa wiki iliyopita ndiyo yaliyomfanya afikishe  10 kwenye ligi.

Kufuatia hali hiyo  Emery anamataka straika huyo wa zamani wa  Borussia Dortmund kuendeleza makali yake na huku akisisitiza kwamba  Aubameyang anaweza kuendelea na moto huo.

“Nataka aendelee kuimarika  na changamoto yake pia ni ya pamoja na ya mtu binafsi,” Emery alisema kabla ya mechi yao ya usiku wa kuamkia leo dhidi ya Manchester United.

“Nataka changamoto yake iwe hiyo kwani ana nafasi ya kuwa mfungaji borwa wa Ligi Kuu England msimu huu. Nataka nimsaidie ili afikie hilo na ni kwamba kwa sababu anapofunga anakuwa ametusaidia sisi,”aliongeza kocha huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*