EMERY AKANUSHA MADAI YA KUWAINGILIA OZIL, LOW

LONDON, England


 

KOCHA wa timu ya Arsenal, Unai Emery, amekanusha taarifa kuwa amemkataza kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low, kuzungumza na mchezaji wake, Mesut Ozil.

Mapema wiki hii, mitandao ya habari ilidai kuwa Low alipigwa marufuku kuongea na kiungo huyo, lakini ilibainika kwamba kocha huyo alimfuata mkuu wa akademi ya Arsenal, Per Mertesacker na si Ozil.

Awali ilidaiwa kwamba, Low na Ozil, walikuwa na mpango wa kumaliza tofauti zilizopo, hasa baada ya kiungo huyo kustaafu soka la kimataifa na wakati huo huo, ripoti nyingine zilimtaja Emery kwamba amemzuia Low kufanya hivyo.

Lakini, Low alitua London kwa ajili ya mazungumzo binafsi na beki wa zamani wa Ujerumani, Mertesacker na kwa wakati huo Ozil hakuwepo mazoezini, huku kocha huyo akizungumza na Wajerumani wengine,  Bernd Leno na Shkodran Mustafi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*