googleAds

Eldorado amshukuru Mr Blue

JEREMIA ERNEST

MSANII anayekuja kwa kasi kwenye Bongo Fleva, John Kunguru ‘Eldorado’, amemshukuru staa wa muziki huo, Mr Blue kwa kukubali kushirikishwa kwenye wimbo, Chechema, unaofanya vizuri kwa sasa.

Akizungumza na Papaso la Burudani jana, Eldorado alisema mwitikio umekuwa mkubwa kutokana na ushirikiano alioupata kutoka kwa Mr Blue, jambo lililompa moyo wa kuendelea kufanya kazi nzuri, akitarajia kuachia wimbo mwingine aliomshirikisha Christina Bella, hivi karibuni.

“Namshuikuru Mr Blue kwa kukubali kufanya ngoma hii, imekuwa na mwitikio mzuri, wadau wamenielewa kwa haraka kuliko nilivyotarajia ingawa bado sijapata uongozi zaidia ya familia yangu kuniunga mkono,” alisema Eldorado.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*