googleAds

Elderado aachia ngoma na Christian Bella

NA ELIAS SIMON

KINDA wa muziki wa kizazi kipya Elderado, ameachia ngoma mpya inayoitwa ‘Nimekuwa’ akiwa amemshirikisha nyota wa muziki wa dansi nchini Christian Bella.

Akizungumza na DIMBA,Elderado alisema, anaamini ngoma hiyo mpya itazidi kumpaisha katika medani ya muziki huo na kujizolea umaarufu.
Hii ni ngoma yake ya pili ya kwanza ni Chechema aliyompa shavu Mr. Blue ambayo bado inatamba katika vituo mbalimbali vya redio.

Chechema imefanya vizuri sana maana Mr Blue ni msanii mkubwa ndani ya Tanzania lakini huu wimbo wa sasa ndio balaa tosha kupitia Christian Bella maana anajua sana sio msanii wa kawaida hapa nchini,î alisema Elderado.

Alisema, anawaomba mashabiki wake waipokee ngoma hiyo kwa kishindo ili kumuongezea hamasa ya kufanya vyema zaidi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*