El Clasico yapigwa kalenda Hispania

CATALUNYA, Hispania

HALI ya usalama imezidi kuwa mbaya katika Mji wa Catalunya nchini Hispania, baada ya wakazi wao kufanya maandamano ya kisiasa yaliyopelekea mchezo wa Barcelona na Real Madrid kusogezwa mbele. 

Shirikisho la Soka Hispania (RFEF) lilifikia makubaliano ya kuahirishwa kwa mchezo huo mkubwa nchini humo kutokana na maandamano hayo ambayo yametibua hali ya amani.

Hata hivyo, taarifa za awali zilidai kuwa viongozi wa Barcelona walikuwa tayari mchezo huo kupelekwa Uwanja wa Santiago Bernabeu hiyo Oktoba 26, lakini ombi hilo lilitupiliwa mbali na RFEF.

Watu 96 wamekamatwa na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa kutokana na maandamano hayo yanayodaiwa kufanywa kisiasa kwa lengo la Catalunya kujitenga na serikali ya Hispania. 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*