googleAds

Ederson kuwakosa Liverpool?

MANCHESTER, EnglandĀ 

KLABU ya Manchester City huenda ikamkosa kipa wao tegemeo, Ederson, baada ya kuumia kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Atalanta, usiku wa kuamkia jana.

Ederson ambaye alijihisi maumivu ya misuli, alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Claudio Bravo.

Kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola, aliweka wazi ana imani na Bravo ambaye huenda akasimama langoni kwenye mechi ya Ligi Kuu England watakaposhuka dimbani kumenyana na Liverpool.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa Italia, Man City ililazimiswa sare ya bao 1-1 na Atalanta huku Bravo akilimwa kadi nyekundu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*