Duu! Kumbe Kidoa alianzia buku 10

NA KYALAA SEHEYE,

VIDEO Queen matata kwenye muziki wa Bongo Fleva, Asha Salum ‘Kidoa’, amesema haikuwa kazi rahisi kuyafikia mafanikio aliyonayo hivi sasa, kwani video yake ya kwanza alilazimika kuifanya kwa malipo ya Sh elfu 10, licha ya ugumu wa kazi.

Kidoa, anayetarajia kuonekana kwenye tamthilia mbili tofauti hivi karibuni, ameliambia Papaso la Burudani kuwa malipo hayo kiduchu yalimkatisha tamaa mpaka pale alipokutana na Ney wa Mitego na kutokea kwenye kichupa cha wimbo uitwao Akadumba.

“Nilikata tamaa na kazi hii, ila namshukuru Ney wa Mitego aliponipa nafasi ya kuonekana kwenye video yake ya Akadumba na kunilipa vizuri nikajikuta narudisha matumaini ya kuendelea kufanya video,” alisema Kidoa, mrembo ambaye hivi sasa amesimama kufanya kazi hiyo labda atokee msanii atakayetenga fungu la kutosha.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*