googleAds

Dull Sykes : Natamani Recho arudi kwenye nafasi yake.

Na RICHARD DEO

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Bongo Flava Abdul Sykes, maarufu kama Dull Sykes amefunguka kuwa ana tamani kumuona mwanamziki Winfirda Josephat ‘Recho kizunguzung’ katika ramani ya muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

Dull Sykes amesema hayo katika mahojiano na moja ya kituo cha Tv, wakati akizungumza maswala mazima ya muziki kwa ujumla na kuzungumzia wimbo mpya ya Recho ujulikanao kama  Chocho.

“Unajua kila siku natamani kumuona Recho akirudi katika nafasi ile ya awali, anajua kuimba tena ni msanii ambaye hana tabia ya kulinga wala kuvimba kwa watu bila kuwa na matabaka ”amesema.

Dull Skyes ni moja ya waasisi wa Bongo Flava ambaye mbaka sasa anafanya vizuri, akitamba na kibao chake kipya cha Weka alicho mshirikisha msanii Marioo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*