Draxler: Kutua Tottenham ndoto za mchana

PARIS, Ufaransa

WINGA wa PSG, Julian Draxler, amesisitiza kuwa hana mpango wa kujiunga na Totteham na kwamba kinachoelezwa ni uzushi mtupu.

Awali, taarifa ziliripoti kuwa Tottenham wanakaribia kumtwaa kwani wameshatuma ofa ya Pauni milioni 27.

“Siwezi kusema chochote kuhusu hilo kwa sababu sina mpango huo na sikuwahi kuzungumza na mtu yeyote,” alisema Draxler.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*