DRAKE APEWA KAZI NBA

LOS ANGELES, Marekani


 

MKONGWE wa mpira wa kikapu, Metta World Peace, amesema rapa Drake anastahili kupewa kazi ya kuinoa Toronto Raptors ya NBA (Ligi Kuu ya Kikapu ya Marekani.

World Peace alisema anaamini kocha anayekalia kiti hicho kwa sasa, Dwane Casey, anapaswa kuonesha mlango wa kutokea na Drake achukue nafasi hiyo.

“Kama (Drake) akipata watu makini, anaweza kabisa,” alisema World Peace katika mahojiano yake na mtandao wa habari za burudani wa TMZ.

“Anatakiwa kufanya hivyo. Ndiyo, nafikiri anatakiwa kufanya hivyo,” alisema World Peace ambaye alitamba NBA kwa misimu 19 kabla ya kustaafu mwaka jana.

Drake amekuwa akionekana katika mechi za timu hiyo kwa miaka mingi sasa na hivi karibuni alihudhuria mchezo wao dhidi ya Cleveland Cavaliers.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*