Dr Cheni afurahia maisha ya U-MC

NA JEREMIA ERNEST

MKONGWE wa filamu nchini na mshereheshaji, Mahsein Awadhi ‘Dr Cheni’, amesema anafurahia kuwa MC  aliyeleta mapinduzi kwenye tasnia hiyo ya kusherehesha kwenye shughuli mbalimbali.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Dr Cheni, ambaye amekuwa Mc katika shughuli za harusi, misiba na nyinginezo alisema washereheshaji wengi wa zamani walikuwa wanaongea sana na kukosa ubunifu.

“Kilichonifanya nipate wateja wengi ni baada ya kubuni mtindo wa kuacha waalikwa wacheze zaidi kuliko kuongea kwa kuwa ile ni siku ya furaha na MC wengi wamekuwa wakiniiga, sifikirii kurudi kwenye filamu sababu soko halijakaa sawa,” alisema Dr Cheni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*