Domayo aenda Sauzi kutibiwa

NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO wa timu ya Azam, Frank Domayo, ameondoka nchini jana kwenda Afrika Kusini kupatiwa matibabu ya msuli wa nyama ya paja ya mguu wa kulia.

Domayo alipata majeraha hayo, wakati alipokuwa katika kambi ya timu ya Tanzania, Taifa Stars, ilipokuwa inajiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la  Mataifa ya Afrika (AFCON), itakayofanyika mwaka  2021 nchini Cameroon dhidi ya Guinea ya Ikweta.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na uongozi wa wa Azam, Domayo ameongozana na daktari wa timu hiyo, Mwanandi Mwankemwa.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa, matibabu ya nyota huyo yatakuwa ya siku 10, kwenye Hospitali ya Vincent Palotti iliyopo jijini Cape Town, nchini humo.

“Nahodha msaidizi wa Azam FC, Frank Domayo ‘Chumvi’, ameondoka nchini alfajiri ya leo (jana) kwenda Afrika Kusini kwa matibabu, tunamtakia kila la kheri katika matibabu yake hayo, aweze kurejea dimbani mapema haraka iwezekanavyo,”ilisema taarifa hiyo.

@@@@@


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*