Dk. Mwakyembe afanya uamuzi ugumu BMT

NA GLORY MLAY

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, amemteua Neema Msitha kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Uteuzi huo umefanyika mara ya Waziri Mwakyembe kukutana na viongozi wa kriketi, wachezaji na wadau wa mchezo huo juzi, Gymkhana, jijini Dar es Salaam.

Waziri Mwakyembe alikutana na wadau hao kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali ndani ya Chama cha Kriketi Tanzania (TCA).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana na Ofisa wa BMT, Frank  Mgunga, Waziri Mwakyembe, ametengua uteuzi wa aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa baraza hilo, Alex Nkenyenge na nafasi yake kuchukuliwa na Neema.

Taarifa hiyo, ilisema kabla ya uteuzi huo, Neema alikuwa ni Ofisa Michezo Daraja la Kwanza na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa baraza hilo.

Wakati huo huo, Waziri Mwakyembe ametengua uteuzi wa Kaimu Msajili wa Vyama vya Michezo nchini, Ibrahimu Mkwawa na kumteua Benson Chacha kuchukua nafasi hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Chacha alikuwa ni Ofisa Michezo Daraja la Pili.

“Kwa mujibu wa sheria na miongozo ya utumishi wa Umma, uteuzi huo unaanza mara moja kuanzia Julai 6, mwaka huu,” imesema taarifa hiyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*