googleAds

DJUMA AMTESA MBELGIJI SIMBA

HUSSEIN OMAR NA AYOUB HINJO              |        


KAMA kuna anayedhani kuondoka kwa Masoud Djuma kutakuwa kumempa ahueni Kocha Mkuu
wa Simba, Patrick Aussems, atakuwa amekosea, kwani kila kitu kinaonekana kwenda ndivyo sivyo kwa Mzungu huyo.

Juzi wakati wa mazoezi
yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterans, Dar es Salaam, Mbelgiji huyo alionekana kutumia nguvu kubwa kuwaelekeza wachezaji wake, kitendo kilichomchukiza na kumlazimisha kuwa mkali mara kwa mara.

Wachezaji wake hawakuwa wakifanya kama alivyokuwa akiwaelekeza, huku tatizo kubwa likionekana kuwa lugha anayotumia.

Ikumbukwe kuwa, Mbelgiji huyo anatumia lugha ya Kifaransa na Kiingereza ambayo ni tatizo kwa baadhi ya wachezaji wa timu hiyo, ukizingatia hakuna kocha anayewatafsiria baada ya kufungashwa virago kwa Djuma, ambaye anafahamu lugha hiyo kama ilivyo kwa Kifaransa na Kiswahili.

Baada ya kubaini ugumu huo, kocha wa makipa wa timu hiyo, Mohammed

Muharami, alilazimika kusogea karibu na Aussems na kumsaidia kuwafafanulia wachezaji maagizo ya Mbelgiji huyo kwa Kiswahili.

Akizungumza na BINGWA baada ya mazoezi hayo, Aussems alikiri kupata wakati mgumu katika kuwanao vijana wake, huku akisisitiza kuwa atapatiwa kocha msaidizi hivi karibuni.

“Kocha msaidizi atakuja hivi karibu, wiki mbili au tatu zijazo, hakutakuwa na tatizo tena,” alisema kocha huyo.

Katika mazoezi hayo, Aussems alionekana kupania na kuwakimbiza vilivyo wachezaji wake kabla ya kuwapa mbinu za ufungaji.

Beki Paschal Wawa alionekana kuzidiwa na zoezi hilo kiasi cha kumfanya kupiga kelele na hatimaye kushindwa kumudu kasi ya mazoezi hayo, hivyo kuishia kuinama, akilalamika kupatwa na maumivu ya kiuno.

Baada ya kuwakimbiza, Ausseme alianza kuwapa mbinu za kufunga wachezaji wake, zoezi ambalo lilidumu kwa zaidi ya saa moja na nusu.

Hivi karibuni, Aussems alisema atakuwa na kazi moja kuwafungia kazi mastraika wake katika suala zima la upachikaji wa mabao.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*