DIAMOND APAA ULAYA, AACHA BALAA BONGO

NA MWANDISHI WETU


NYOTA wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, leo anatarajia kuungana na mastaa wengine wa muziki barani Afrika katika tamasha la One Africa linalofanyika katika Uwanja wa SSE Arena Wembely, Uingereza.

Tamasha hilo ambalo huwakutanisha wasanii wa Afrika na mashabiki zao wanaoishi Uingereza, huku mwaka huu mastaa kama Cassper Nyovest, Banky W, Vanessa Mdee, 2 Face, Eddy Kenzo, Nasty C, Mr Flavour, K CEE, Tekno na wengine wengi watatumbuiza.

Wakati hayo yakiendelea, wimbo Iyena ambao Diamond Platnumz ameutoa usiku wa kuamkia jana, umeendelea kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya Zari The Boss kuonekana akifunga ndoa na staa huyo.

Video hiyo ambayo ilifanyika Agosti mwaka jana, imewafanya mashabiki wa Zari akiwamo mama na dada wa staa huyo, kummwagia sifa mama Tiffah kuwa ana vigezo vyote vya kuwa mke wa Diamond Platnumz.

Kwa habari zaidi pata nakala yako ya gazeti la BINGWA hapo juu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*