googleAds

DIAMOND AMFUATA ZARI AFRIKA KUSINI, WAPEANA MAHABA

NA CHRISTOPHER MSEKENA

BAADA ya kukiri kuchepuka na mwanamitindo, Hamisa Mobetto, kwenye uhusiano wake imara na Zarina Hassan ‘Zari The Boss Lady’, msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemfuata mama watoto wake Afrika Kusini na kumwomba msamaha.

Katika kile kinachoonekana kuwa Zari The Boss Lady amemsamehe Diamond Platnumz na kumpa ruhusa ya kujumuika naye kwenye sherehe yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa iliyofanyika juzi Afrika Kusini, wawili hao walionekana kwenye video wakiponda raha kimahaba.

“Uzuri na urembo pengine ningetembea nikakuta baadhi wanao pia lakini akili, hekima pamoja na roho yako ya kwenye shida na raha, kwangu ndicho kitu pekee kinachonifanya nikupende na kukuthamini zaidi kadiri siku zinavyozidi kwenda…… wanaposema kwenye kila mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke imara nyuma, hawamaanishi eti anayepika na kuosha vyombo sana ama kufua nguo kila siku… hapana! ni mwanamke mwenye kuwa bega kwa bega na mpenziwe kwenye shida na raha… Happy birthday General,” aliandika Diamond Platnumz kwenye ukurasa wake wa Instagram akimtakia heri ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Zari The Boss Lady.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*