googleAds

Diamond aiteka Guinea Bissau kwa muda

NA MWANDISHI WETU

STAA wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, ameisimamisha kwa muda nchi ya Guinea Bissau katika onyesho lake lililofanyika Uwanja wa Estádio Lino Correia, unaojaza watu zaidi ya 5,000.

Diamond alitua nchini humo Ijumaa iliyopita na kupokewa na maelfu ya mashabiki waliokaa nje ya Uwanja wa Ndege wa Osvaldo Vieira wakimsubiri kisha kuongozana naye katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Bissau na kusababisha watu wasimamishe kazi zao kwa muda.

“Vuta picha uwanja wa ndege umejaa hivi, kwenye nchi ambayo wanaongea ‘Ki-portuguese’ (Kireno), hawajui Kiswahili wala hawaongei Kingereza, siwezi kuelezea niwashukuru vipi,” alisema Diamond.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*