Dembele afungua njia kwa wanaomtaka

PARIS, Ufaransa 

MSHAMBULIAJI wa Lyon, Moussa Dembele ametaka kurejea Ligi Kuu England, na kujiunga na timu yoyote itakayomuhitaji kwa mujibu wa ripoti.

Timu hizo zilizotajwa ni Manchester United na Everton, ambazo zinamfuatilia kwa ukaribu mshambuliaji huyo.

Itakumbukwa Dembele aliwahi kukipiga Fulham msimu wa 2012-2013 kabla ya kuondoka na kujiunga na Lyon.

Dembele ameonyesha kiwango kizuri msimu huu huku akiwa amefunga mabao sita katika mechi 10 alizocheza kwa mashindano yote.

Kwa mujibu wa ripoti, Everton wameweka pauni milioni 20 (sh bil.50) ya kumnasa itakapofika dirisha dogo la usajili Januari. 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*