googleAds

D’banj ametoswa lebo ya Kanye West?

LAGOS, Nigeria

MWANAMUZIKI mwenye jina kubwa Nigeria, D’banj, ameelezwa kusitishiwa mkataba wake na lebo ya muziki ya G.O.O.D Music, inayomilikiwa na staa wa muziki wa hip hop kutoka Marekani, Kanye West.
Kilichozua shaka kuwa huenda D’banj ametemwa ni kitendo cha lebo hiyo kutoa orodha ya majina ya wanamuziki wao, huku lile la nyota huyo likikosekana.

Kwa mujibu wa orodha hiyo, wasanii wanaotambuliwa na G.O.O.D music ni Kanye West, Big Sean, Desiigner, John Legend, Pusha T, Tyga, Teyana Taylor, Kacy Hill na Q-Tip.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*