googleAds

DAH! ETI P-SQUARE IMEVUNJIKA

LAGOS, Nigeria

IMERIPOTIWA kuwa kundi la muziki la P-Square, linaloundwa na mapacha Paul na Peter Okoye limevunjika na huenda ukawa ndio mwisho wa uhondo wa kuwaona wawili hao wakiwa pamoja jukwaani.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, Peter ndiye aliyeamua kuondoka kwenye kundi hilo lenye umaarufu mkubwa kweye soko la muziki barani Afrika.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, Peter anatajwa kukerwa na kitendo cha Paul kufuta ziara ya Marekani bila kuwasiliana naye.

Lakini pia, inadaiwa kuwa amemshutumu ndugu yake huyo, akimtaja kumtukana mke na mtoto wake kwenye mitandao ya kijamii.

Ikaelezwa kwamba jamaa aliandika barua kwa mwanasheria wao aitwaye Festus Keyamo, akiomba kutotambuliwa kama mhusika wa P-Square.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*