CURRY AWEKA REKODI NBA

LOS ANGELES, Marekani


 

NYOTA wa Golden State Warriors ya Ligi Kuu ya Kikapu (NBA), Stephen Curry, amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga pointi tatu mara tano katika michezo saba mfululizo.

Curry mwenye umri wa miaka 30, alifanya hivyo alfajiri ya jana wakati alipoiongoza Warriors kuitandika Brooklyn Nets kwa pointi 120-114.

Mchezo huo ulimalizika kwa mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu (MVP), kutupia pointi 35.

Mkali huyo ameuanza kwa kasi ya ajabu msimu huu kwani katika mechi zote saba alizocheza, hajafunga chini ya pointi 29.

Alitia fora zaidi katika mechi dhidi ya Washington Wizards mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo alifunga pointi tatu mara 11.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*