COUTINHO AWATABIRIA MAKUBWA SALAH, NEYMAR

 MADRID,Hispania


 

KIUNGO wa Barcelona, Philippe Coutinho, amesema kwamba anavyoamini  mastraika Mohamed Salah  na  Neymar  watatisha katika fainali za Kombe la Dunia zikazoanza hvi karibuni nchinniu Urusi.

Wawili hao wanatarajia kwenda katika mashindano hayo wakiwa majeruhi, baada ya  Salah kuumia bega katika mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa na huku Neymar akiwa jacheza muda mrefu baada ya kuvunjika mguu Februari mwaka huu.

Hata hivyo, Coutinho, ambaye aliwahi kucheza na Salah  wakiwa Liverpool kabla ya Januari mwaka huu kuhamia  Barcelona   na ambaye amekuwa akicheza na Neymar  katika safu ya ushambuliaji ya timu ya Taifa ya Brazil, anasema kuwa mastaa hao wanaweza kuwafunika hata Lionel Messi  na  Cristiano Ronaldo wakati wa fainali hizo.

 “Kwa sasa nadhani ni mawazo ya kila mmoja kufanya vizuri wakati wa fainali za Kombe la Dunia,”alisema  Coutinho.

“Messi  na  Ronaldo  wamekuwa wakitamba kwa  miaka mingi. Nadhani sasa ni wakati wa wachezaji wengine kufanya vizuri duniani na katika fainali za Kombe la Dunia,”alisema staa huyo.

“Kwangu mimi, Salah  na  Neymar wana nafasi kubwa ya kufanya hivyo. Ingawa itategemea na jinsi mashindano yatakavyokwenda, lakini wana kipaji cha kufanya hivyo,”alikwenda mbali zaidi nyota huyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*