googleAds

Corona yawaibua Wawa, Lamine mitandaoni

NA MWAMVITA MTANDA

LIGI Kuu Tanzanian Bara, ikiwa imesimama kwa kwa siku 30, kutokana na tahadhari ya virusi vya Corona, mashabiki wa Simba na Yanga, wamehamia kuwajadili mabeki wao, Pascal Wawa na Lamine Moro mitandaoni.

Kundi la mashabiki wa Simba na Yanga, juzi liliposti kwenye mtandao wa facebook majina ya mabeki hao wakitaka kujua nani anamzidi mwenzake kiwango cha soka.

Hata hivyo, Lamine alifanikiwa kumshinda Wawa kwa ubora, baada ya kuongoza kwa kura 108 za maoni ya mashabiki hao dhidi ya 76 alizopata beki huyo wa Simba.

Akizungumza na BINGWA, mmoja wa mashabiki wa Yanga, Yasin Jiwe, alisema Wawa ni beki mzuri lakini kwa sasa hana kasi kama ya ile ya Lamine kutokana na umri wake.

“Mimi ni Yanga damu, lakini nilikuwa namuelewa sana Pascal Wawa kwa kipindi cha nyuma, lakini ukweli ni kwamba Lamine ni chuma, wenyewe Simba wanajuta kwa nini walimuacha,” alisema Jiwe.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*