Corona yapeperusha rufaa ya Tanzania CAF

NA ZAINAB IDDY

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF), limeshindwa kusikiliza rufaa ya Tanzania dhidi ya Uganda kutokana na tishio la virusi vya Corona.

Tanzania iliwasilisha rufaa CAF, ikidai Uganda kuwachezesha wachezaji waliozidi umri katika michuano ya wasichana wenye umri chini ya miaka 17 ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

Katika mchezo huo wa marudiano uliochezwa hivi karibuni, kwenye Uwanja wa Star Times, Kampala, wenyeji Uganda waliibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Matokeo hayo yaliiwezesha Uganda kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-2, baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Tanzania kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Akizungumza na BINGWA jana jijini, Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Oscar Mirambo, alisema rufaa yao iliwasilisha kwa kamati husika ya CAF.

“Tumerejeshewa majibu kuwa rufaa yetu imepokelewa, lakini haitafanyiwa kazi kutokana na janga la Corona lililojitokeza ambalo linasababisha kutokuwapo kwa vikao  pamoja na vipimo mbalimbali kushindwa kufanyika.

“Matumaini yetu baada ya siku 30 zilizozuiwa mikusanyiko kumalizika na janga hili kupungua, CAF watasikiliza rufaa  na haki itatendeka kwa sababu ushahidi tunao kuwa Uganda walitumia wachezaji wanne waliozidi umri wa miaka 17  kitu ambacho ni kinyume na sheria za mashindano,” Milambo


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*