Corona yamzuia Deo Kanda kuona familia

NA MWAMVITA MTANDA

MSHAMBULIAJI wa pembeni wa timu ya Simba, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Deo Kanda, amesema ameshidwa kwenda kuona familia yake kutokana na tishio la virusi vya Corona.

Kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imesimama kwa muda kutokana na janga hilo, ambao linaendelea kutikisa Dunia.

Akizungumza na BINGWA jana, Kanda alisema anahofia nchini kwao kwa sababu anaweza kupata  virusi vya Corona akiwa njiani na kuathiri familia yake.

Kanda alisema Corona ni virusi hatari na mpaka sasa anaona jinsi alivyotenganishwa na familia yake, kwani hali ingekuwa shwari angeweza kwenda kuwaona.

“Nilitamani sana kuondoka jijini Dar es Salaam, lakini nimeona kusafiri pia ni hatari hasa ukiangalia namna ya  ugonjwa wenyewe unavyoambukizwa, naweza kujikuta nimeupata njiani na kuteketeza familia yangu, nipo hapa mpaka hali iwe shwali.

“Mara nyingi huwa naongea nao kwa simu kutambua hali zao, watoto wapo salama hawatoki nyumbani kama ilivyo hapa Tanzania,” alisema Kanda.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*